• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

TIMIZENI WAJIBU WENU KATIKA MALEZI YA WATOTO KUJENGA FAMILIA BORA: KANALI AHMED ABBAS AHMED.

Posted on: May 15th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa malezi kwa watoto hatua ambayo amesema itapunguza vitendo vya mmomonyoko wa maadili na hivyo kujenga familia bora zenye upendo zinazotatua matatizo yake kwa njia ya mazungumzo ili kutoa fursa kwa wazazi na watoto kuyapatia ufumbuzi.

Kanali Abbas ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la Siku ya kimataifa ya familia lililofanyika katika ukumbi wa Chuo  cha Ualimu Ufundi mjini Mtwara na kusisitiza kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kutambua umuhimu wa familia na mchango wake maendeleo ya jamii na uchumi wa taifa jambo ambalo litapata tija kwa kuwashirikisha wadau kuanzia nagazi ya familia waweze kujadili na kupanga mikakati ya utekelezaji.

Aidha, Kanali Abbas amewakumbusha wazazi kutekeleza msingi wa malezi hasa kwa kujua na kutimiza majukumu yao ya kuwalinda watoto katika maeneo ya msingi ikiwemo kuwatimizia mahitaji yao ya  msingi, kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili sambamba na kuzungumza nao moja kwa moja ili  kutambua changamoto zinazo wakabili na maendeleo yao kwa ujumla.


Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii, Mkoa wa Mtwara Bi  Tabitha kilangi amesema kuwa Maadhimisho ya Siku ya familia duniani yanalenga kuhamasisha, kuhimiza, kuelimisha na kuiamsha  jamii kuhusu umuhimu wa familia ili iweze kuchukua hatua stahiki katika kuimalisha na kuendeleza familia.

Halikadhalika Bi kilangi amewataka washiriki kuitekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya Maadhimisho hayo inayosema “Imarisha Maadili na Upendo kwa Familia imara” hatua ambayo itamsukuma kila mwanafamilia kuwajibika kwa nafasi yake ikiwemo kutenga muda wake wa kukaa na familia ikiwa ni pamoja na kuwapatia malezi mema watoto.

Maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya familia mkoani Mtwara yalihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi wa kawaida, wadau kutoka taasisi za kiraia pamoja na viongozi wa dini ambapo wamejadili na kuweka mikakati kuhusu namna ya kuimarisha malezi bora katika ngazi ya familia kama njia ya kuepukana na wimbi la vitendo vya ukiukwaji wa maadili katika jamii.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2022 November 24, 2021
  • Majina ya watumishi wa umma wanaostahili kulipwa madai ya malimbikizo February 09, 2018
  • KUFANYA MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19 August 30, 2021
  • Matokeo ya Kidato cha NNe 2017 January 30, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • NI JUKUMU LETU VIONGOZI KUIELIMISHA JAMII UMUHIMU WA CHANJO - KANALI AHMED ABBAS AHMED_MKUU WA MKOA WA MTWARA.

    July 20, 2023
  • JIANDAENI KUTEKELEZA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 – KANALI AHMED ABBAS AHMED_MKUU WA MKOA WA MTWARA.

    July 19, 2023
  • SERIKALI KUENDELE KUWASHIKA MKONO WAATHIRIKA WA MAJANGA , MILIONI 231 ZATUMIKA – MHE. JENISTA MHAGAMA

    July 17, 2023
  • TUNATEKELEZA ILANI KWA VITENDO - DANIEL CHONGOLO_KATIBU MKUU CHAMA CHA MAPINGUZI.

    July 16, 2023
  • Tazama Zote

Video

Wakulima Mtwara wachangamkia kilimo cha Ufuta
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • NBS
  • IKULU
  • UTUMISHI
  • SALARY SLIP
  • e-GA

Kurasa Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.