Kuelekea mwaka mpya wa Mahakama nchini tarehe 5 Februari 2026, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala ameshiriki maadhimisho ya siku ya Sheria nchini, ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya mahakama kuu Mtwara. Maadhimisho hayo yamefanyika leo tarehe 02 Februari 2026 yakiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe.Jaji Edwin Kakolaki.
"Nchi yenye amani na utulivu, inakaribisha wawekezaji na kuiletea maendeleo, nitoe rai kwa wadau wote wa haki na madai, kutoa haki mapema na bila kuchelewesha" Ameeleza Kanali Sawala.
Jaji Kakolaki ameeleza kuwa mahakama itaendelea kutoa haki bila upendeleo kama ambavyo Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inataka utawala bora na haki kuwa kipaumbele muhimu katika kufikia maendeleo ya Taifa.
"Haki ikicheleweshwa, wananchi watakosa imani na mahakama hivyo kuchelewesha maendeleo na ustawi wa wananchi." amesema Jaji Kakolaki.
Aidha amesema kuwa mahakama imeendelea kujiimarisha katika eneo la teknolojia, ambapo hivi sasa mashauri yanasikilizwa kwa njia ya mtadao hali inayochangia kuharakisha utolewaji wa haki.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.