Wilaya ya Nayumbu ilitangazwa rasmi kuwa Wilaya na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Benjamin William Mkapa, tarehe 29/07/2005. Makao Makuu ya Wilaya ni Mji wa Mangaka.
Wilaya ya Nayumbu ina ukubwa wa kilometa za Mraba 5071.5 sawa na asilimia 30 ya eneo lote la Mkoa wa Mtwara.
Wilayah hii inapakana na wilaya ya Nachingwea kwa upande wa kaskazini, Wilaya ya Masasi kwa upande wa Mashariki, Jamhuri ya Msumbiji upande wa Kusini na Wilaya ya Tunduru upande wa Magharibi.
Wilaya inapata mvua za kati ya 400mm na 832mm kwa mwaka na wastani wa joto ni kati ya nyuzi joto 250C na 320C.
Kwa Mjibu wa Sensa ya Kitaifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Wilaya ilikuwa na jumla ya wakazi wapatao 150,857 (wanawake 72,237 na wanaume 78,620). Ongezeko la watu ni wastani wa asilimia 2.1 kwa mwaka. Pato la mwananchi wa Wilaya ya Nanyumbu linakadiriwa kuwa Tshs 442,572 kwa mwaka.
Zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa Wilaya ya Nanyumbu wanategemea kilimo kwa ajili ya kujipatia chakula na mapato. Mazao ya biashara yanayolimwa ni Korosho, Ufuta, Karanga, Choroko na Mbaazi. Mazao ya chakula ni Mahindi, Mpunga, Muhogo, Mtama, Mbaazi, NjuguMawe, Kunde na Upupu.
Fursa za uwekezaji zilizoko katika Wilaya ya Nanyumbu ni pamoja na
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.