MKOA WA MTWARA

OFISI YA MKUU WA MKOA WA MTWARA
news menu left news menu right
top news photography KARIBU MKOA WA MTWARA

Kwa niaba ya wananchi wa Mtwara,ninapenda kuwakaribisha katika Mkoa wa Mtwara,unafikika kirahisi kwa njia ya barabara,maji na anga. Mkoa wa Mtwara una fursa nyingi za uwekezaji,hivyo kuwa sehemu ya uwekezaji inayokuwa kwa kasi.Hii inatokana na mazingira mazuri ya kijiografia,kiuchumi na kibiashara yaliyopo katika Mkoa. ----Mh.col(Ret) Joseph Simbakalia

Wanaotazama Tovuti

We have 1 guest online

Barua Pepe

Home

MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOA WA MTWARA

Picha: Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh Joseph Simbakalia akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh Mwambungu

Mkoa wa Mtwara kwa Mwaka huu ulipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Ruvuma ambao ulipokelewa na Mhe. Kanali (Mst) Joseph Simbakalia, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara siku ya tarehe 13/11/2011 katika Kijiji cha Lumesule Wilaya ya Nanyumbu.

Mhe. Kanali (Mst) Simbakalia aliukabidhi Mwenge huo wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatma Ally na ndipo mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Mtwara zikaanza rasmi.

Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Mtwara ulitembelea jumla ya miradi 10 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.7 katika Wilaya za Nanyumbu na Mtwara. Kati ya miradi hiyo, miradi 7 iliwekewa jiwe la msingi, 2 ilifunguliwa na 1 ulikaguliwa.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Mtumwa R. Khalfani, pia alitoa mikopo kwa wajasiriamali 10 wa vikundi mbalimbali katika Wilaya ya Nanyumbu.

Pamoja na kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru Mwaka huu ya “Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi Kusonga Mbele”, pia uliangazia na kusisitiza mambo makuu matatu ambayo ni mapambano dhidi ya UKIMWI, Madawa ya kulevya na Rushwa.

Miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka huu ni pamoja na kuweka jiwe la msingi katika ghala ya kuhifadhia mazao, mradi wa ujenzi wa nyumba 50 za PSPF, ujenzi wa madarasa matatu, ujenzi wa nyumba ya mganga, ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho, ujenzi wa wodi ya wazazi na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa soko la samaki.

Miradi mingine ni ufunguzi wa nyumba ya kulala wageni, ghala la kuhifadhia mazao na kukagua banda la madawa ya kulevya, upimaji hiari VVU, banda la vijana wajasiriamali na banda la kuzuia na kupambana na rushwa.

Baada ya kutembelea miradi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Hasna Mwilima aliukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mhe. Kanali (Mst) Simbakalia na ndipo Risala ya Utii ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete iliposomwa.

Katika Risala hiyo wananchi wa Mkoa wa Mtwara walitoa shukrani kwa Mhe. Rais kwa jitihada anazozichukua kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa Mkoa wa Mtwara na Tanzania kwa ujumla. Pia waliunga mkono juhudi zake za mapambano dhidi ya Rushwa, UKIMWI, Dawa za Kulevya na ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), jitihada za utetezi wa haki za wanawake, watoto na uimarishaji wa huduma za Jamii.

Vilevile Mhe. Rais alipongezwa kwa kuanzisha mchakato wa uundaji wa Katiba mpya kwa kuwashirikisha wananchi katia hali ya amani na utulivu. Wananchi wa Mkoa wa Mtwara walitoa ahadi ya kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo na kudumisha amani, utulivu na umoja kwani ndani ya miaka 50 ya Uhuru Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi kusonga mbele.

Siku ya tarehe 15/11/2011 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na viongozi mbalimbali waliukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Lindi katika Kijiji cha Madangwa, Lindi Vijijini.

 

 

HABARI ZA SASA

TEMBELEA




Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

d yaviagra